Wakati umewadia! Shule zimefunguliwa!
Twajua una malengo makubwa kwa ajili ya mwanao. Unataka ang’are! Afanye vizuri. Afanikiwe! Hivyo basi, tumekuandalia mbinu hizi TANO zitakazomsaidia mtoto wako afanikiwe si tu shuleni, bali pia katika kila afanyacho!
1. Soma naye!
Keti na mwanao msome pamoja! Someni vitabu, pitieni magazeti, zungumzeni! Mwulize maswali kuhusu mnachosoma. Kusoma mara kwa mara humpa mtoto msingi imara wa LUGHA, utakaofanya awe na uwezo wa kujieleza kwa ufasaha na kufanya watu wamuelewa katika chochote atakachofanya maishani. Kusoma pamoja kutafanya pia uwe karibu na mwanao!
2. Huko shule anafanya nini?
Kila anapotoka shule, piga naye stori! Mwulize siku yake imeendaje, na amejifunza nini. Usiulize tu alichofanya, bali mwambie AKUELEZEE hicho alichosoma siku hiyo! Hii ni mbinu nzuri ya kuhakikisha anafanya marudio, na hukuonyesha pia maeneo ambayo anahitaji msaada!
3. Zungumza na mwalimu wake kila mara!
Ongea na walimu wake mara kwa mara! Fahamu maendeleo ya mwanao! Je, anafanya vizuri kama mwalimu wake anavyotaka? Anahitaji msaada? Keti na mwalimu mpange mikakati ya kumsaidia mtoto wako afanye vizuri shuleni!
4. Fahamu anachopenda!
Mwanao anapenda hesabu? Ana shauku ya kujifunza zaidi Kiswahili, ama Kiingereza, au kuchora? Mtie moyo kila anapofanya mazoezi ya masomo haya. Lakini pia usisahau kutazama maeneo mengine anapohitaji msaada zaidi!
5. Mfanye apende kujifunza!
Tengeneza mazingira yanayofanya mtoto wako afurahie kujifunza, hasa pale anapotoka shule. Cheza naye michezo mbali mbali! Undeni vitu pamoja! Tumieni teknolojia kujifunza! Fanya yale yanayomsukuma mwanao atumie #akili!
Mpatie mwanao msingi IMARA wa ELIMU kwa kutumia app zetu za BURE, zinazopatikana kwa KIINGEREZA na KISWAHILI. Zitamwezesha ajifunze herufi na maneno mapya katika mazingira yanayomfurahisha na kumburudisha!